Tukilichunguza tatizo hili kwa muhtasari tunaona kwamba tabia ya ukeketaji
imejengeka katika mila na imani za watu kufuatana na mazingira yao. Mila
na imani zinazohusiana na ukeketaji zina madhumuni au makusudi fulani
yanayotakiwa kufikiwa na jamii husika. Kwa mfano ukeketaji una
madhumuni yafuatayo:-
Kumwondoa msichana kutoka rika la utoto na kuingia utu uzima.
Kumzuia msichana asiwe na tamaa ya kujamiiana na wanaume ovyo
ovyo.
Mahari- wazazi wenye watoto waliokeketwa wanayo nafasi kubwa ya
kupata mahari kubwa kwa ajili ya watoto wao.
Kuongeza raha ya mwanamume katika tendo la ndoa
Kuondoa ugumba, magonjwa ya kizazi nuksi na mikosi, n.k.
Kumtawala mwanamke (mfumo dume) na mengine yafanayo na hayo.
NAHII SIO HAKI !